JAMII YATAKIWA KUWAUNGA MKONO WASAIDIZI WA SHERIA MAPAMBANO YA UDHALILISHAJI

  



NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@

JAMII imetakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, katika kupiga vita vitendo vya mbali mbali vya kihalifu vikikiwemo vile vya ukatili na udhalilishaji.

 

Wakitoa elimu juu ya kuviepuka vitendo hivyo kwa wanafunzi Januari 23, 2025 wa Madrassatul Nuru-lhuda ya kijiji cha Tondooni shehiya ya Wesha, wasaidizi hao wa sheria walisema watendaji wa vitendo hivyo hufanyaji siri, na ndio maana nguvu za pamoja na zinahitajika.

 

Walisema, kama juhudi zinazofanywa na wasaidizi wa sheria zitaungwa mkono na jamii, kunauwezekano mkubwa kwa kiasi falani matendo hayo kupungua, kwani watendaji wanaishi kwenye jamii.

Akitoa mada juu ya udhalilishaji msaidizi wa sheria kutoka shehiya ya Mgogoni wilayani humo, Jaffar Abdalla Ali, alisema watendaji hutumia mbinu mbali mbali, kabla ya kuwadhilishaji watoto ikiwemo kuwapa zawadi.

 


Alieleza kuwa, ni vyema watoto kwa sasa wakawa na utamaduni wa kutoa taarifa watakapogundua kuna mtu anawanyemelea ikiwemo kuwapa pesa na zawadi nyingine katika maeneo yasio rasmi.

 

‘’Kwa mfano watoto msikubali kupokea zawadi kama pesa, pipi na hata msaada wa usafiri aidha kwa mtu msiyemjua au mnemhisi ana tabia mbaya,’’alisisitiza.



Katika hatua nyingine Msaidizi huyo wa sheria, aliwakumbusha wazazu na walezi kuwa, iwapo atatokezea mtoto kukumbwa na udhalilishaji, sio vyema kusafishwa au kukogeshwa, kwani ni sehemu ya kupoteza ushahidi.

 

‘’Ikitokezea bahati mbaya mtoto kabakwa ama kalawitia, harakisheni kumfikisha, kituo cha Mkono kwa mkono au Polisi, ili ushahidi ukae vyema,’’alisisitiza.

Mapema Msaidizi wa sheria kutoka shehia ya Wesha Khadija Said Khalfan, aliwakumbusha wazazi na walezi, kuwaangalia watoto kwa kina, ili kujua ikiwa wanamichezo michafu ama laa.



‘’Njia nzuri ya kugundua, ikiwa mtoto wako anadhalilishwa ama alaa, kwa wale wadogo ni kupendelea kuwakogesha, japo wiki mara mbili, mana wapo wingine huharibiwa na mzazi kuchelewa kujua,’’alifafanua.

 

Kwa upande wake msaidizi wa sheria kutoka shehiya ya Wawi Haji Nassor Mohamed, aliwataka wazee wa watoto wanao soma katika Madrasa hiyo, kufuatilia nyenendo za watoto wao, ili kuwaweka katika mazingira salama yakuepukana na udhalilishaji.  



Mwanafunzi Naifat Massoud Ali na mwenzake Zulhulaifat Fadhil Rashd, waliwataka wanafunzi wenzao, kuacha kuwaita watu majina ambayo hawataki, kwani kufanya hivyo ni moja ya udhalilishaji.’

 

Akifunga mkutano huo wa wazi, Mwalimu mkuu katika Omar Rajab Ali, alisema mpango wa ulioanzishwa na CHAPO wa kuwafuata wananchi kuwapa elimu na mzuri na unafaa kuendelezwa.



Kwa mwaka huu tayari wasaidizi hao wa sheria kutoka CHAPO, wameshazitembelea shehia za Mgogoni, Wesha, Wara na Wawi na zaidi ya wannachi 150 wameshafikishiwa elimu ya kisheria.

Mwisho

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’