CHAPO: YAKABIDHI MSAIDIZI WA SHERIA SHEHIA YA MGOGONI

  


NA MWANDISHI MAALUM, PEMBA@@@@

WASAIDIZI wa sheria kutoka Jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’ wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na jamiii, ilikuondosha migogoro kwa njia ya kuiripoti katika sehemu zinazohusika kisheria.

Hayo yameelezwa Januari 21, 2025 na wajumbe wa kamati wa sheha wa Mgogoni wilayani humo, mara baada ya kumtambulisha Msaidizi wa sheria Jaffar Abdalla Ali, anayetarajiwa kufanyakazi katika shehia hiyo, hafka iliyofanyika kijiji cha Mgogoni.

 


Walisema kuwa katika shehia hiyo, kumekuwa na matukio mengi ambayo hayana mshughulikiaji wa moja kwa moja kisheria, hali inayopeleka watu wengi kukosa haki zao kutokana na kukosa eneo husika la kuzidai.

 

Akimtambulisha msaidizi huyo wa sheri, kiongozi wa timu ya wasaidizi wa sheria, kutoka Jimbo la Wawi Haji Nassor Mohamed, aliwaambia wajumbe hao kuwa, kufanyakazi kwa karibu na Msaidizi huyo wa sheria.

 Alisema, kwa muda mrefu shehia hiyo ilikosa Msaidizi wa sheria wa moja kwa moja, hali iliyokuwa ikiwapa changamoto wajumbe hao na wananchi kwa ujumla.



‘’Sasa CHAPO imekuleteeni Msaidizi wa sheria, ambae anapaswa kufanyakazi ndani ya shehia ya Mgogoni, sasa mtumieni kila inapobidi,’’alishauria.

Kwa upande wake Naibu sheha wa shehiya hiyo Khadija Ramadhan, alisema katika shehiya hiyo zipo changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa njia za kitaalam, hivyo kupitia Msaidizi huyo sheria, zinaweza kupata mwarubaini.

Nae Msaidizi wa sheria anayetarajiwa kufanyakazi shehia ya Mgogoni, Jaffar Abdalla Ali, alisema jambo kubwa linalohitajika ni ushirikiano kutoka kwa wajumbe hao.



Alieleza kuwa, atatumia nguvu zote katika kutoa elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa wananchi wa Mgogoni, ili kuona vitendo vya kihalifu vinapungua.

 

‘’Mimi nimeshakabidhiwa kwenu, kilichobakia sasa ni kunishirikisha na kunipa ushirikiano wa hali ya juu, maana ili Mgogoni isiyo na uhalifu inawezekana kama tukishirikiana,’’alieleza.

Akizungumza katika hafla hiyo, mjumbe wa sheha Mariam Juma Salim, aliahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu, kwa Msaidizi wa huyo wa sheria, ili kuhakikisha Mgogoni inakuwa salama.





Kwa upande wake Msaidizi wa sheria, Fatma Hilali Salim, alimuahidi Masaidizi huyo wa sheria, kuendelea kumpa ushirikiano wa hali ya juu, ili kufikia lengo lao.

 

Msaidizi huyo wa sheria ya Mgogoni, ameunganishwa kwenye timu ya wasaidizi wa sheria kutoka shehia za Wesha, Wawi na Wara, ili kufanyakazi kama timu moja.

MWISHO

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’