MSAIDIZI MPYA WA SHERIA JIMBO LA WAWI AKARIBISHWA
NA AMINA AMHED, PEMBA::
UONGOZI wa Shehia ya Wawi Jimbo
la Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba, umesema utatoa kila
aina ya ushirikiano na msaidizi wao mpya wa sheria, katika kutatua
changamoto mbali mbali za jamii zikiwemo matukio ya ukatili na udhalilishaji wa
kijinsia, ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikikosa ufumbuzi, kwa kutokuwepo
msaidizi wa sheria.
Hayo
yalielezwa Januari 22, 2023 na Sheha wa Shehia ya Wawi Sharifa Ramadhan Abdalla, alipokuwa
akifungua mkutano maalum wa kutoa Elimu kwa wajumbe wa sheha wa shehia
hiyo, kutoka kwa Msaidizi moya wa sheria Kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria
wilaya ya Chake Chake Pemba 'CHAPO'.
Alisema
anaamini kuwa Idara ya Katiba na Masaada wa Kisheria kumuwezesha Msaidizi huyo
wa sheria, haikukosea, kwani amemuwa mtendaji mzuri na mfuatuliaji hata kabal
ya kupata mafuanzo ya awali ya sheria na sasa kuijiunga na CHAPO na kuwa
katika shehi hayo.
Alisema kwa
anavyomfahamu Msaidizi huyo wa sheria, naamini zile chhamgamoto mbali mbali
ikiwemo kero la udhalilishaji, ambazo zinaendelea zinajitokeza
katika vijiji vilivyomo ndani ya shehia hiyo, vinakwenda kupungua kwa
kasi shehiani humo.
Sheha huyo
alieleza kuwa, kilichobakia kwa jamii na wajumbe wa sheha ni kumpa ushirikiano
wa dhati Msaidizi huyo wa sheria ili aendelee kuisaidia jamii katia majanga
mbali mbali na hasa wizi, udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya.
''Kwanza
sisi uongozi wa shehia ya Wawi tumefarajika kwa elimu uliyotupa na tunajivunia
kuwa na Msaidizi wa sheria wewe, maana kila mmoja anajua utendaji wako wa kazi
na ufuatialiaji wako na sisi tutakupa ushirikiano wa hali na mali,''alieleza.
Katika hatua
nyingine sheha huyo wa shehia ya Wawi, alisema kama jamii ikishirikiana kwa
moyo wa kweli, hakuna ovo wala uhalifu wa wowote utakaoshinda ndani ya shehia
ya Wawi.
"Uwepo
huu wa Msaidizi wa sheria ndani ya shehia hii ya Wawi, itakuwa ni msaada
mkubwa kwa wananchi, katika kutatua baadhi ya kesi hasa za madai, kwani
zipo ambazo huishia kienyeji ni kutokana na kukosa msaada wa kisheria katika jamii,''alisema
sheha huyo.
Akizungumza katika mkutano huo Msaidizi huyo wa sheria jimbo la Wawi kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake Chake CHAPO. Haji Nassor Mohamed, alisema kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa shehia, Msaada wa kisheria utawafikia wananchi katika maeo mbali mbali tena bila ya malipo.
Alisema kuwa,
sasa yuko tayari kutumwa na wananchi wenzake, ili kutoa elimu ya kisheria,
ushauri na msaada bila ya malipo, kwani ndio msingi mkuu wa upatikanaji haki
kwa jamii ya jimbo la Wawi.
Msaidizi huyo wa
sheria alieleza kuwa, Idara ya Katiba na Msaada wa sheria ilitumia gharama
kubwa kumuwezesha, sasa hana budi kutimiza malengo ikiwa ni pamoja na
kuitumikia jamii wakati woowte.
Hata hivyo
ameuomba uongizi wa shehia ya Wawi na jimbo kwa ujumla kumpa ushirikiano wa
hali na mali, ili kufanikiisha kuifikia jamii, katika kupata na kutetena haki
zao.
''Inawezekana
jamii yetu imeshakata tamaa kufuatilia haki zao katika vyombo vya sheria, sasa
uwepo wangu mimi na tukishirikiana hatua kwa hatua tunaweza kufikia malengo na
kuirejeshea serikali imani kwa wananchi wake,''alieleza.
Alisema, msaidizi
huyo wa sheria anamfahamu vyema utendaji wake wa kazi tokea akiwa mwandishi wa
habari, sasa kilichobakia kwa wananchi wa Jimbo la Wawi ni kumtumia ili
kushirikiana katika utatuzi wa changamoto mbali mbali.
''Kwanza niseme kuwa, kwa changamoto tulizonazo shehia ya Wawi na aina ya Msaidizi wa sheria tulienae kama tutashirikiana zitapungua kwa kiwango kikubwa mno,''alifafanua Mjumbe huyo wa Bodi ya CHAPO.
Nao baadhi
ya washiriki wa Mkutano huo akiwemo Mjumbe wa sheha wa shehia hiyo
katika kijiji cha Wawi Mtemani Nassor Rashid aliwataka
wananchi wa Wawi kutodharau Viongozi wa Shehia wanapofikwa na changamoto
mbali mbali na kukimbilia vyombo vikubwa kabla kupitia katika
uongozi wa shehia ili kuepusha Mivutano isiyoya lazima.
Katika mkutano
wajjumbe hao wa shehe wamefundishwa nini maana na ushahidi, aina za ushahidi,
sababu za kutoa ushahidi, changamnoto kwa mashahidi, nani mtoto kisheria na
changamoto katika kuendesha kesi za udhalilishaji kwa watoto wenye miaka katia
ya 15 hadi 17 mahakamani.
Mwisho.




Comments
Post a Comment