‘CHAPO’ YATIMIZA AHADI KWA WANAMICHEZO WAWI
NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
WANAMICHEZO
shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, wametakiwa kujiepusha na matumizi ya vilevi
kama vile dawa za kulevya, kwani kufanya hivyo, wanaweza kuzima ndoto zao
mapema kwenye michezo.
Ushauri huo umetolewa na Msaidizi wa sheria wa shehia hiyo
Fatma Hilali Salim, Septemba 9, 2025 shehiani humo, wakati akizungumza na wanamichezo
hao na wananchi wingine, kwenye hafla ya kukabidhi mipira, iliyotolewa na Mkurugenzi
Idara ya Katiba na Msaada wa sheria pamoja na Katib Mtendji wa Baraza la Vijana
Zanzibar.
Alisema, moja ya njia nyepesi kwa mwanamichezo yeyote ili
asifikie ndoto zake kwenye michezo, ni matumizi ya dawa za kulevya, ambazo ni
hatari kwa afya yake.
Alieleza kuwa, dawa za kulevya sio tu kwamba zinazima ndoto
kimichezo, lakini zinamshushia heshima, kutoonekana binaadamu kamili,
kutoaminika katika jamii yake.
‘’Dawa za kulevya kwa mwanamichezo ni sumu ya kutokusonga
mbele, maana hao munaosiki ni wachezaji wakubwa, walianza kuwa afya njema, ndio
kisha wakafanikiwa,’’alisema.
Akizungumzia umuhimu wa michezo, alisema ni kupata ajira,
kujenga uhusiano na watu wingine, kujuana, kuzidisha umaarufu na kuwa na afya njema.
Hata hivyo, aliwakumbusha wazazi na walezi, kuendelea
kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, ili kutoa taarifa za kihalifu, katika
shehia yao.
Katika hatua nyingine Msaidizi huyo wa sheria shehia ya Wawi
Fatma Hilali Salim, aliwakumbusha wanachi hao, kutodharau mikutano, kwani
wanaweza kupoteza haki zao.
Mapema Msaidizi wa sheria shehia ya Mvumoni Haji Nassor Mohamed,
aliwaasa wananchi hao, kuendelea kuwatumia wasaidizi wa sheria, wanapokuwa na
changamoto ya masuala ya kisheria.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipra hiyo, alisema Hanifa Ramadhan
Said, ambae ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar,
aliahidi kuchangia mipira mitatu kwa ajili ya vijana wa Wawi.
Alisema, yeye alichangia mipira hiyo, ili kuhakikisha wanapiga
hatua mbele ya kimichezo, ili wasipate muda wa kukaa kwenye vijiwe, ambavyo ni
kichecheo cha uhalifu.
Kwa upande wake Katib wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar
‘ZFF’ ofisi ya Pemba, Khamis Hamad Juma, akiwasilisha kanuni za mpira wa miguu,
alisema ni kujenga heshima wakati wa michezo.
Jingine ni afya njema, kushinda, kukubali kushindwa, nidhamu,
kusaidia kushinda, michezo wa kuridhiana, heshima mambo ambayo ndio msingi wa
uwepo wa michezo.
Sheha wa Wawi Khamis Mohamed Khamis ‘bin jaa’, aliwashukuru,
Hanifa Ramadhan Said ambae ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa
kisheria na Katib Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar, Ali Haji Hassan, kwa
kutimiza ahadi zao.
Katibu wa klabu ya Wawi Star Ali Salim ‘babu lii’ alisema,
mipira hiyo wataitumia kwa kuendeleza mbele ushindi na ushindani, kwa timu
nyingine.
‘’Kwanza niwashukuru wasaidizi wa sheria na wakuu wao, kwa
kutimiza ahadi yao kwetu na sisi tunawaahidi mipira hii minne itakuwa sehemu ya
kupata ushindi,’’alifafanua.
August, 9 mwaka huu, ujumbe wa Idara ya Katiba na Msaada wa
kisheria ukishirikiana na wasaidizi wa sheria, ulifika shehiani humo na kuendesha
mkutano wa elimu ya haki binaadamu kwa wananchi hao.
MWISHO

Comments
Post a Comment