'WALINDENI WATOTO NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA'
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANANCHI
wa kijiji cha Birikau shehia ya Michungwani wilaya ya Chake chake Pemba,
wametakiwa kuwalinda watoto wao, kwani watumiaji, wasafirishaji na waingizaji
wa dawa za kulevya, wamekuwa wakiwatumia watoto, katika kufanikisha malengo
yao.
Ushauri huo
umetolewa April 30, 2024 na Askari kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Chake chake, anayezifanyia
kazi shehia za Wesha, Michungwani na Ndagoni wilayani humo Khamis Ali Khamis, wakati
akizungumza na wananchi, kwenye mkutano wa wazi.
Alisema, kwa
sasa watumiaji na wasafirishaji wamekuwa wakiwatumia watoto, wakijua kuwa,
kisheria hawashatakiwa na wakati mwingine hawawezi kupekuliwa.
Alieleza kuwa,
taarifa zipo zinazoenesha kuwa, sasa watoto wamekuwa wakitumiwa na watumiaji,
wasaambazaji wa dawa za kulevya, baada ya mitego ya kuwatumia watu wazima
kugundulika.
‘’Wazazi wa
kijiji ch Birikau, kuweni makini mno na wasambaazaji, watumiaji, wauzaji na
waingizaji wa dawa za kulevya, sasa wamehamishia kazi hiyo kwa watoto,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine Askari huyo wa shehia, aliwataka wazazi na walezi hao, kufufua malezi
ya pamoja miongoni mwao, ambapo kufanya hivyo wanaweza kuwakinga na majanga
watoto wao.
‘’Leo kila
mmoja ni shahidi kuwa, watoto wamekuwa na ugumu kwenye malezi, sasa
tusiporejesha malezi yale ya zamani, ya kuhakikisha tunaleleana watoto, majanga
yanaweza kuwa mingi kwao,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine Askari huyo, aliwataka wananchi hao kutoa taarifa wakati wowote katika
vyombo husika, wanapoona viashiria vya vijana wanaotaka kutumia dawa za kulevya.
Mapema Msadizi
wa sheria wa shehia za Wesha, Michungwani na Ndagoni Khadija Said Khalfan,
aliwakumbusha wazazi na walezi hao, kukaa na watoto wao kila wakati, ili
kuwagundua ikiwa wameanza kudhalilishwa ama laa.
Alieleza kuwa,
wazazi wasipokuwa karibu na watoto wao, wanaweza kukumbwa na majanga ya udhalilishaji
na kuchelewa kuwagundua, ikiwa wameanza kufanyiwa vitendo hivyo.
Wakati huo
huo, Msaidizi huyo wa sheria amewataka wananchi kuwatumia wasaidizi wa sheria
kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria CHAPO, waliomo shehiani mwao, wanapokuwa
na changamoto za kisheria.
‘’Njooni
kwetu mpate ushauri na msaada wa kisheria bila ya malipo, kwani moja ya jukumu
letu ni kuhakikisha wananchi waliopoteza mwelekeo wa kupata haki zao, wanasaidiwa,’’alieleza.
Mmoja wa mzazi
wa kijiji hicho, Salama Makame Haji, alisema elimu bado inahitajika kwa jamii,
juu ya namna kutoa taarifa wanapoona viashiria vya udhalilishaji.
Nae mwananchi
Hamza Salum Khamis, alisema kama sheria inaukubali ushahidi wa picha, katika
makosa ya jinai, imekuwa jambo zuri kwao, katika kutokomeza makosa hayo.
Katika hatua
nyingine Mwalim wa Almadrassatul Jazzira Islammiya ya Birikau Ali Othman
Mohamed, amewakumbusha wazazi na walezi, kuwabidiisha watoto wao, juu ya suala
la kuhudhuria madrassa.
Akifungua mkutano
huo, Mwalimu wa Almadrassatul Zainabiya sheikh Mohamed Omar Mussa, amesema elimu
waliyoipata watahakikisha wanaifanyia kazi, ili jamii ipate mabadiliko.
Mwisho
Comments
Post a Comment