WATOTO WASAKATA SOKA WESHA WALALAMIKIA KUTENGWA MATUMIZI YA UWANJA
BARAZA la watoto wa shehia ya Wesha wilaya ya Chake
chake Pemba, wamesema changamoto yao ya kukatazwa matumizi ya uwanja wa mpira wa
miguu nyakati za jioni, inawanyima fursa ya kujiendeleza, kimichenzo.
Walisema kuwa,
changamoto hiyo inawarudisha nyuma kimichezo, kwani hawapati muda mzuri katika kufanya
mazoezi yao.
Hayo,
yameelezwa na mjumbe wa kamati hiyo, Saidi Mohamed Ali, kwenye mkutano wa wazi,
uliyoandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake chake (CHAPO),
uliofanyika huko Wesha kwa Sheha.
Alisema,
watoto katika kijiji chao, wana malengo makubwa
katika soka, kutokana na kuwa, mpira siku hizi ni ajira na biashara pia.
Alisema kuwa, vijana wengi siku hizi wamefanikiwa
kujipitia ajira kupitia soka, hivyo nao kuendelea kubanwa na timu kubwa
wasifanye mazoezi, kwenye uwaja pekee
uliopo Wesha, ni kuanza kuzizima ndoto zao.
‘’Kila
mmoja asubuhi anakwenda kwenye harakati, sasa jioni ndio wakati wa mazoezi,
lakini inapokuja timu kubwa, ambayo chanzo ni sisi wadogo, hutukufukuza,’’alieleza.
“Mpira siku
hizi ni ajira, na Serikali yetu, ina malengo makubwa na vijana, katika
kutuendeleza kisoka, lakini sisi tunanyimwa hiyo fursa na timu kubwa, katika
uwanja wetu,’’alilalamika.
Nae,
Samir Magesi alisema anatamani siku moja
kuwa mchezaji wa timu kubwa kama Simba na Yanga, ingawa changamoto ya kuzuiwa kutumia
uwanya wa mpira wa miguu, wakati wa jionii inawarejesha nyuma.
Alisema kuwa,
soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla limekuwa, lakini vijijini bado hakuna viwanja
kwa watoto, vya kufanyia mazoezi, ili kujijenga kimichezo.
“Huku
kwetu, vijijini watoto hatuna viwanja vya kufanyia mazoezi, ndio maana tunavizia
kiwanja cha wakubwa, na sisi kufanya mazoezi, ingawa wenyewe ni wakali,”
alisema.
Aidha, aliiomba Serikali ya Mapinduziya Zanzibar kuwajengea viwanya vizuri na watoto wa vijijini ili kukuza vipaji vyao.
Nae msaidizi
wa sheria kutoka Shehia ya Wawi, Haji Nassor Mohamed aliwaahidi kuifanyia kazi changamoto
yao hiyo, ikiwa na pamoja na kuwaahidi vifaa vya michezo.
Aliwataka,
wasikate tamaa, kutokanana changamoto inayowakabili, katika kujiendeleza kimichezo
na kufanya bidii ili kufikia malengo yao kimichezo.
MWISHO
Comments
Post a Comment