CHAPO YAWAONESHA NJIA WANA WAWI KUEPUKA MIGOGORO YA ARDHI

 


 

NA ASHA ABDALLA, PEMBA

WANANCHI wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake, wametakiwa kutafuta hatimiliki kutoka serekalini, maratu baada ya kununua kiwanja,  shamba au kipande cha aina yoyote cha ardhi, ili kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima.

 

Hayo yameelezwa Oktoba 28, 2023 na Mjumbe wa Bodi kutoka Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’ Asha Sleiman Said, wakati akizungumza na wananchi hao, kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na jumuiya hiyo na kufanyika Kunguni Wawi.

 

Alisema kua, zipo njia mbali mbali zinazotumiwa ili mtu aweze kupata haki ya kutumia ardhi bila ya migogoro yoyote, ikiwemo njia yakununua na kupewa hati ya matumizi.

 


Alieleza kuwa, migogoro mingi ya ardhi husababishwa na watu kukosa hati za matumizi pamoja na kuwekeana mipaka inayoondoka kama vile miti na mifimbi ya mito na maziwa.

 

Mjumbe huyo kutoma CHAPO, alifahamisha kuwa, mwarubaini pekee mara baada ya mtu kununua, kupewa hiba, kurithi, kuiomba serikalini ni kufuatia hati za umiliki serikalini.

 

"Kuna maeneo mbali mbali ambayo tumefanya zoezi la kutoa hati za umiliki wa ardhi, kupitia zoezi la la utambuzi na usajili wa ardhi, lakini hata baada ya hati kukamilika, watu hawazichukui,’’alieleza.

 

Nae Msaidizi wa sheria sheia ya Wawi Haji  Nassor Mohamed, alisema wasaidizi washeria wana nafasi kubwa katika suala zima la kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuzilinda haki za binaadamu.

 



Alisema kua haki moja na muhimu ya binaadamu ni ile ya kuishi, ambayo hakuna mwenye mamlaka ya mwengine kumuondolea mtu haki hiyo.

 

‘’Ndio maana hapa tunapinga vikali suala la watu kujichukulia sheria mikononi kwa muua mtuhumiwa wa wizi wa ndizi, kuku na Ng’ombe kwa madai ya vyombo vya sheria kutokuchukua hatua,’’alieleza.

 

 Akizungumzia haki ya kupata Habari, aliwataka wananchi hao wasidharau mikutano hiyo, na waposi”ia upatu ama njia nyingine yeyote ya taarifa kufika haraka kwenye mikutano inayoitishwa.

 

Kwa upande wake Askari shehia kutoka kituo cha Polisi Madungu Chake chake, Issa Ahmada Iddi, alisema kua, wananchi  wanapopatwa na matukio mbali mbali, waepuke kujichukulia sheria mikononi mwao, kwani vyombo vya ulinzi vipo.

 



 Hata hivyo aliwakumbusha wananchi hao, kufufua ulinzi ushirikishi, ambao kwa baadhi ya shehia kama vile Mkoroshoni wamefanikiwa kudhibiti matendo ya uhalifu.

 

Mwananchi wa shehiya hiyo Omar Juma Khamis alitoa ushauri kwa serekali, wanapokwenda kupima ardhi ambayo wanataka kutoa hatimiliki, wapime sehemu zote nne na wahusika wawepo kushuhudia.

 

Sheha washehiya hiyo Sharifa Waziri Abdalla, alisema kua watajitahidi kuchukua taaluma hiyo walioipata, na kuwapa wenzao, ili kuondokana na changamoto zinazojitokeza za migogoro ya ardhi na uvunjifu wa haki za binadamu.

 




Msaidizi wa sheria shehia ya Wawi na Mgogoni Fatma Hilali Salim, alisema wanaendelea kutoa ushauri, elimu na msaada wa sheria bila ya malipo kwa wanancho wote.

 

 MWISHO

 

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’