WAWI WAUKUBALI USHAURI WA MSAIDZI WA SHERIA UJENZI WA OFISI YA SHEHA
NA MWANDISHI WETU, CHAPO@@@@
UONGOZI wa shehia ya Wawi wilaya ya
Chake chake, umesema umeridhia usahuri wa Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi,
la kutaka kuanzisha ujenzi wa ofisi ya sheha, shehiani humo.
Ulisema,
wazo la Msaidizi wa sheria wamelipokea mikono miwili, kwani imekuwa ni usumbufu
wanapokuwa na mikutano yao mbali mbali, hasa katika kipindi cha jua au mvua.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, leo Juni 16, 2023 Sheha wa shehia hiyo Sharifa Waziri Abdalla, alisema
baada ya kulifikisha wazo hilo kwa wajumbe wake, wamelipokea na kusema linawezekana
mno kutekelezwa.
Alisema, fikra
hiyo imekuja wakati mwafaka, wakati serikali kuu nayo ikihimiza ujenzi wa ofisi
za masheha, ili sasa waondokane na kufanyakazi kwenye makaazi yao.
Alieleza kuwa,
wazo hilo ambalo aliahidi kulisimamia, linaweza kutekelezwa, hasa kwa umoja na
mshikamano, uliopo ndani ya shehia ya Wawi.
‘’Ni kweli
tumeupokea na kuukubali ushauri wa Msaidizi wetu wa sheria wa Jimbo la Wawi, la
kuomba kuanzishwa kwa ofisi ya sheha, maana inaweza kuwa chachu ya mafanikio,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, sheha huyo wa shehia ya Wawi, aliwataka wajumbe wake kuusambaaza
ujumbe huo kwa wananchi, ili wakati wa kuataka kuanza ujenzi ukifika wawe na
uwelewa.
Aidha sheha
huyo alimpongeza Msaidizi huyo wa sheria kwa ujio wa wazo hilo, na kusema
amesaidia katika kuleta mabadiliko ya haraka ndani ya shehia.
Akizungumzia
kushirikiana na Msaidizi huyo wa sheria, aliwataka wananchi kuendelea kumtumia,
kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa masuala mbali mbali ya kisheria.
‘’Kama kuna
migogoro kama ya ardhi, matunzo, huduma za mtoto, mipaka, madeni kuendelea
kushirikiana nae, ili kufikia sulhu, badala ya kwanza kukimbilia Polisi,’’alieleza.
Mjumbe wa
sheha wa kijiji cha Mtemani Nassor Rashid Said, alisema kilichobakia kwa
wananchi wa shehia ya Wawi, ni kusimama wima juu ya ujenzi huo.
‘’Hili jambo
alilolita Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi, ni zuri na linafaa kuungwa
mkono, na kwetu sisi ni kufanya ufuatiliaji,’’alishauri.
Nae mjumbe
wa sheha Khamis Mwinjaa, aliwata wajumbe wenzake, kuendelea kushirikiana kwa
karibu, ili kuijenga shehia yao.
Kwa upande
wake Mratibu wa wanawake na watoto shehia ya Wawi Fatma Kassim, alisema ofisi
hiyo itakapojengwa, itatoa nafasi pana wakati wa kutoa ushauri nasihi, kwa
wahanga wa udhalilishaji.
‘’Hivi sasa inabidi
wahanga tunakaa nao barazani kuwapa ushauri nasihi, lakini kama kuna wazo la ujenzi
wa ofisi, litasaidia mno, katika kusukuma mbele maendeleo,’’alieleza.
Wakizungumza kwa
niaba ya wasaidizi wa sheria wenzake, Haji Nassor Mohamed na Asha Hilali, walisema ni kweli hivi
karibuni, waliishauri Kamati ya sheha wa shehia ya Wawi, juu ya kuanzisha ofisi
hiyo.
‘’Tuliona vikao
vya sulhu vinafanyika barazani kwa sheha, uwanjani, au wakati mwengine kwenye
majengo ya kiimani ya kichama, tukaona sio sahihi,’’walieleza.
Wasaidizi
hao wa sheria walisema, wazo hilo wanatarajia litafanyiwa kazi, ili kuona shehia
ya Wawi, inakuwa na ofisi yake kwa ajili watendaji, kuendesha kazi zao kwa ufanisi.
Mkurugenzi
wa Jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, CHAPO Nassor
Bilali Ali, alipongeza wazo la wasaidizi hao wa sheria, jimbo la Wawi kwa
kufikisha wazo hilo shehiani.
Alieleza kuwa,
wasaidizi wa sheria wamepelekwa kwa maksudi shehiani, ili kwenda kusaidia
utatuzi wa changamoto mbali mbali za kisheria, pamoja na upatikanaji huduma
mbali mbali kwa njia ya mashauriano.
‘’Ni kweli
pamoja na majukumu ya msingi ya Msaidizi wa sheria kutoa elimu, ushauri na
msaada wa kisheria, lakini kama kuna ushauri wa kufanikisha mambo mengine,
inakubalika,’’alieleza.
Hata hivyo
Mkurugenzi huyo, amewataka wasaidizi wengine wa sheria, kuwa wabunifu katika
shehia zao, ili wananchi waendelee kupunguza changamoto.
Katika hatua
nyingine Mkurugenzi huyo, aliushauri uongozi wa shehia ya Wawi, kufikiria ikiwa
eneo litatosha, kuanzisha chumba cha Msaidizi wa sheria na Mratibu wa wanawake
na watoto.
Tayari uongozi wa shehia ya Wawi, umeanza harakati za kutafuta eneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo, sambamba na kutaka kuteua kamati ya muda ya ujenzi.
Mwisho
.jpg)




Comments
Post a Comment