WASAIDIZI WA SHERIA WAWI: 'VIJANA MSICHEZE CHEZE NA WATOTO OVYO OVYO WATAWAUMBUA'

 



NA MWANDISHI MAALUM, CHAPO

MSAIDIZI wa sheria Jimbo la Wawi Haji Nassor Mohamed, amewatahadharisha vijana wa shehia ya Wawi, kuacha kucheza cheza na watoto, kwani huwa rahisi kuwataja mara wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Kauli hiyo ameitoa Febuari 19, 2023 uwanja wa mpira wa miguu Wawi, wakati akizungumza na wanamichezo kabla ya kuanza kwa michezo ya ligi daraja la pili taifa, mkoa wa kusini Pemba.

Alisema ule utamaduni wa kucheza cheza na watoto wa kike na wakati mwengine kuwaita majina kama mchumba, wauwepuke, kwani wapo vijana ambao umeshawawek pabaya, baadhi ya watu.

‘’Kama kuna mtoto wa miaka 12, au 16 hadi 17 umekuwa ukipenda kumtania kwa kumuita mchumba, hili jambo tuwe makini nalo, maana mtoto akidhalilishaji na mtu asiyemju, huwa rahisi kumtaja aliyekaribu naye,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, Msaidizi huyo wa sheria Jimbo la Wawi Haji Nassor Mohamed, amewaelekeza wanamichezo hao, kuwa kisheria mtoto ni mtu yeyote aliyechini ya miaka 18.





‘’Kwa mujibu wa sheria zetu, mtoto hana ridhaa, hivyo hata kama yeye atakuita kwao na kukufungulia mlango, lakini mkifanya tendo, hutafsiriwa kuwa ni ubakaji,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, amewataka wanamichezo hao kushughulika na michezo na kazi nyingine za kujipatia kipato cha halali, na sio kujiingiza kwenye vitendo vya wizi.


Hata hivyo amewataka kila mmoja kuwa mlinzi kwa mwenzake, juu ya matumizi, kusambaaza, kuuza au kuingiza dawa za kulevya, kwani madhara yake ni makubwa.

Amewakumbusha kuwatumia wasaidizi wa sheria waliomo jimboni humo, ili kupata ufumbuzi wa mambo yao mbali mbali ya kisheria.

Mapema Katibu klabu ya mpira wa miguu ya Wawi star Juma Mohamed ‘Mgawaji’ alisema aliwakumbusha vijana hao, kujiepusha na visharia vyote vinavyowapeleka kwenye matendo ya kihalifu.


‘’Kama tuna msaidizi wetu wa sheria tumtumieni tunapokuwa na shida kwenye masuala ya kisheria, iwe jinai au madai, ili kupata ufumbuzi kabla ya kwenda juu zaidi,’’aleleza.

Kwa upande wake Msaidizi wa sheria wa Jimbo hilo Fatma Hilali, aliwasisitiza vijana hao, kujiheshimu na kuheshimiana, ili kulinda haki za binadamu.

‘Inapoishia haki yao ya bindamu, ndio inapoanzia ya mwenzako, sasa lazima hili tulijue ili kuhakikisha tunaishi kwa amani,’’alieleza.

Nae Mjumbe wa sheha wa shehia hiyo kutoka kijiji cha Mtemani shehia humo, Nassor Rashid Said, alimtaka Masaidizi huyo wa sheria, kuendelea kukutana na vijana kila wakati, kuwapa elimu kama hiyo.

‘’Sheria ni jambo pana na kubwa, sasa tukuomba leo isiwe ya mwisho, maana vijana wanakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja dawa za kulevya, udhalilishaji na wizi,’’alifafanua.

                                 Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’