Posts

Showing posts from September, 2026

WAJUMBE KAMATI YA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI MVUMONI, YAPIGWA MSASA

Image
  NA SAIDA ALI, PEMBA@@@ WAJUMBE wa Kamati ya Kupambana na Udhalilishaji ya shehia ya Mvumoni wilaya ya Chakechake, wametakiwa kuendelea kuielimisha jamii, madhara ya ukatili na udhalilishaji, kwa wanawake na watoto. Wito huo umetolewa leo Septemba 26, 2026 na Afisa Elimu wilayani humo, Burhan Khamis Juma, wakati akiyafungua mafunzo ya siku moja, ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hiyo. Alisema, bado kamati za kupinga udhalilishaji hasa za ngazi ya shehia, zitaendelea kuwa msingi mkuu, kwa jamii katika kupata elimu ya kupinga udhalilishaji. Alieleza kuwa, kamati hizo ambazo zipo kisheria, zinatakiwa kuendelea kuielimisha jamii, madhara ya muda mfupi na mrefu ya udhalilishaji. ‘’Niombe kamati ya kupambana na udhalilishaji, kuendela kuielimisha jamii, juu ya namna bora ya kujikinga na viashiria vya ukatili na udhalilishaji, hasa kwa wanawake na watoto,’’alifafanua. Katika hatua nyingine Afisa Elimu huyo, aliipongeza kamati ya kupambana na udhalilishaji ya wilaya ya Cha...